CHAN 2020: Tanzania yaiondoa Kenya katika michuano hiyo ya Afrika

Mshambuliaji wa Taifa Stars Mbwana samata wakati wa michuano ya Afcon Misri

Chanzo cha picha, CAF

Timu ya kandanda ya taifa Stars kutoka tanzania imeiondoa timu ya harambee Stars kutoka kenya katika mashindano ya CHAN 2020

Timu ya Kenya Harambee Stars ilidondoka katika michuano ya kufuzu kombe la CHAN 2020 baada ya kupoteza kwa Tanzania taifa Stars 4-1 kupitia mikwaju ya penalti katika uwanja wa Kasarani jijini Nairobi baada ya kutoka sare 0-0 katika dakika 90 za mchezo.

Mkufunzi wa Harambee Sebastien Migne alichagua washambulia waliokuwa na kasi akiwemo Samuel Onyango na Duke Abuya lakini hawakuweza kucheka na wavu, na ilipofikia majira ya penalti Taifa Stars ilithibitisha kwamba wao ndio magwiji watakaoelekea Camroon ambapo michuano hiyo itachezwa mwezi Januari.

Harambee Stars walikuwa wametoka sare ya 0-0 siku ya Jumapili iliopita mjini Dar es Salaam na kufuatia ushindi huo Taifa Stars sasa itakutana na Sudan katika raundi ya pili na ya mwisho ya kufuzu.

Safu ya mashambulizi ya Harambee Stars ilionyesha ukakamavu wa mashambulizi lakini hawakuweza kufua dafu mbele ya safu ya ulinzi iliowekwa na Taifa Stars.

Joash Onyango alionyesha umahiri wake katika safu ya ulinzi ya Kenya na kuzuia hatari iliokuwa ikisababishwa na Jonas Mkudde.

Safu ya mashambulizi ya Harambee Stars ilionyesha ukakamavu wa mashambulizi lakini hawakuweza kufua dafu mbele ya safu ya ulinzi iliowekwa na Taifa Stars.

Joash Onyango alionyesha umahiri wake katika safu ya ulinzi ya Kenya na kuzuia hatari iliokuwa ikisababishwa na Jonas Mkudde.

Iddi Alli alikosa bao la wazi kufuatia uvamizi wa Taifa Stars katika lango la Kenya baada ya Isuza kupokonywa mpira.

Kipindi cha kwanza kiliisha kwa sare tasa lakini Harambee Stars ilikaribia kufunga katika kipindi cha pili baada ya Miheso wa Kenya kuvamia lango la taifa Stars.

Tanzania ilikaribia kufunga kupitia mshambuliaji wake Mkudde lakini ulinzi mzuri wa Miheso ulimzuia mshambuliaji huyo matata.

Kunako dakika za mwisho Mkudde alivamia tena lango la Harambee Stars baada ya kumpokonya mpira Oyemba wa Kenya na kusalia na goli lakini mshambuliaji huyo mrefu wa Tanazania akapiga nje.