Pata taarifa kuu
USHIRIKIANO-DIPLOMASIA

Rais wa Jamhuri ya Afrika ya Kati Touadéra azuru Ufaransa

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron anampokea mwenzake wa Jamhuri ya Afrika ya Kati Faustin-Archange Touadéra siku ya Jumatano kujadili "hali nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, katika ukanda pamoja na masuala tofauti ya uhusiano wa nchi hizo mbili", imesema ikulu ya Elysée.

Rais wa Jamhuri ya Afrika ya Kati Faustin-Archange Touadéra, Septemba 17, 2021 mjini Bangui.
Rais wa Jamhuri ya Afrika ya Kati Faustin-Archange Touadéra, Septemba 17, 2021 mjini Bangui. © Carol Valade / RFI
Matangazo ya kibiashara

Wawili hao walikuwa tayari wamekutana huko Elysée miezi sita iliyopita kuashiria nia yao ya kuungana tena baada ya miaka mingi ya mvutano. Katika miaka ya hivi karibuni, Ufaransa imeshutumu ushawishi unaoongezeka wa kundi la mamluki la Urusi la Wagner nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, ikilishutumu kwa mauaji ya raia na uporaji wa maliasili.

Paris pia ilichukizwa na kampeni za upotoshaji ambazo zilichochea chuki dhidi ya Ufaransa katika nchi hii na kwingineko. Utawala wa Bw. Touadéra "unakandamiza mashirika ya kiraia, vyombo vya habari na vyama vya siasa vya upinzani", shirika la kimataifa la haki za binadamu la Human Rights Watch (HRW) pia iliandika mnamo Aprili 2023, ikitoa "wasiwasi mkubwa juu ya hatari katika suala la ukiukwaji wa haki za binadamu na kupunguzwa kwa nafasi ya kidemokrasia na uhuru wa kujieleza. .

Bw. Touadéra alibadilisha Katiba mnamo Julai 2023 kwa kura ya maoni iliyosusiwa na upinzani, ili kujiidhinisha kugombea muhula wa tatu mwaka wa 2025. Alichaguliwa mwaka wa 2016 katikati ya vita vya wenyewe kwa wenyewe, alichaguliwa tena 2020 katika mazingira tatanishi wakati upinzani ukipinga kuchaguliwa kwake na katika nchi ambayo sehemu kubwa ya eneo hilo ilidhibitiwa na waasi, ambao jeshi lake liliwarudisha nyuma kutokana na usaidizi wa Moscow na uingiliaji kati mkubwa wa mamluki wa Wagner.

Jamhuri ya Afrika ya Kati ni mojawapo ya nchi zinazozungumza Kifaransa barani Afrika ambapo Paris imeshuhudia ushawishi wake ukipingwa na Urusi. Baada yake, Mali, Burkina Faso na Niger pia zilijitenga na Ufaransa, huku Urusi ikianzisha ushirikiano wake na nchi hizo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.